#Local News

WETANG’ULA AMFUNGIA  NDINDI NYORO VIKAO BUNGENI KWA SIKU TANO

Spika wa Bunge Moses Wetang’ula amemsimamisha Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kuhudhuria vikao vya Bunge kwa siku tano, baada ya kutoa madai kuhusu mchakato wa kubinafsisha kampuni ya Kenya Pipeline.

Adhabu hiyo itaendelea hadi Nyoro atakapoondoa madai yake na kuomba msamaha kuhusu tuhuma za ukiukaji wa taratibu katika mchakato huo.

Nyoro alikuwa amedai Rais William Ruto alipiga simu kwa wakuu wa mashirika ya serikali yakiwemo NSSF na Kenya Re, kuwaagiza kuwekeza katika Kenya Pipeline, akisema fedha za pensheni hazifai kuwekeza kupitia maagizo ya simu za kisiasa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *