KINDIKI ATAKA IDARA YA MAGEREZA KUZINGATIA SERA ZA KITAIFA
Naibu Rais Kithure Kindiki ameitaka Idara ya Huduma za Urekebishaji Tabia kuzingatia sera za kitaifa katika kutekeleza mpango wake wa mabadiliko na kuboresha utoaji wa huduma.
Akizungumza jijini Nairobi wakati wa kufungua rasmi wiki ya nne ya huduma za urekebishaji tabia, Kindiki amesisitiza umuhimu wa taasisi hizo kuimarisha matumizi ya teknolojia.
Amezitaka taasisi hizo kuoanisha mipango yao ya kidijitali na mpango wa kitaifa wa kidijitali wa 2022 hadi 2032, mkakati wa biashara mtandaoni na mkakati wa kitaifa wa akili unde wa 2025 hadi 2030.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































