#Athletics #Sports

KIPCHOGE AWEKA REKODI MPYA MELBOURNE

Gwiji wa mbio za marathon Eliud Kipchoge ameshinda mbio za Melbourne nchini Australia akiwa na umri wa miaka 41, akiweka rekodi mpya ya mashindano hayo kwa saa 2 dakika 9 na sekunde 10.

Mshindi huyo mara mbili wa dhahabu ya Olimpiki alipata ushindi wake wa kwanza wa marathon tangu Berlin mwaka 2023, akiwapita wapinzani wake wa Australia katika hatua za mwisho za mbio hizo za Jumapili.

Huu ni ushindi wa 17 wa marathon katika taaluma yake, huku Kipchoge akivunja rekodi ya awali ya Melbourne kwa sekunde mbili katika mara yake ya kwanza kushiriki mashindano hayo na kumalizia mbio katika uwanja wa Melbourne Cricket Ground.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *