LEOPARDS YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU
AFC Leopards imeanza kupata nafuu katika ligi kuu ya soka nchini baada ya kuilaza Kenya Police mabao mawili kwa moja katika uwanja wa Nyayo .
Kevin Luke Otiala aliwafungia Ingwe bao la kwanza dakika ya 49, kabla ya Elvis Rupia kusawazisha kwa Kenya Police kufuatia pasi ya Edward Omondi.
Leopards ilipata bao la ushindi katika dakika za nyongeza kupitia Ronald Sichenje, na hivyo kujinyakulia ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuanza kwa sare tasa dhidi ya Bandari.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































