#Local News

SIFUNA ATANGAZA AZMA YA KUMKABILI RUTO 2027

Seneta wa Nairobi na kiongozi wa Linda Mwananchi, Edwin Sifuna, ametangaza rasmi azma ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 dhidi ya Rais William Ruto.

Akizungumza katika Kanisa la Jesus Teaching Ministry, Sifuna amepuuzilia mbali wasiwasi kuhusu uzoefu na uwezo wake wa kifedha, akisema lengo lake ni kuhakikisha serikali ya sasa inatawala kwa muhula mmoja pekee.

Sifuna amesisitiza kuwa upinzani unahitaji kuungana chini ya mwavuli mmoja ili kuepuka kugawanya kura na kuongeza nafasi ya kuishinda serikali katika uchaguzi ujao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *