SIFUNA AIBUA MJADALA WA KISIASA KATIKA MAADHIMISHO YA RAILA
Vigelegele vya kumshangilia Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha Raila Odinga mjini Bondo vimeibua mjadala kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa chama cha ODM na ushawishi wake katika eneo la Nyanza.
Maelfu ya waombolezaji walikusanyika katika uwanja wa Migwena, kumuenzi Raila, ambaye kwa miaka mingi alikuwa na uhusiano mkubwa wa kisiasa na eneo hilo pamoja na chama cha ODM
Mapokezi aliyopata Sifuna, yameibua maswali kuhusu uhusiano wa ODM na wafuasi wa Raila pamoja na uwezo wa chama kudumisha umoja baada ya kifo cha kiongozi huyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































