WIZARA YA AFYA IMEFANYA MASHAURIANO NA SEKTA YA AFYA KUHUSU HATUA ZA KUKABILIANA NA EBOLA
Wizara ya Afya imefanya mashauriano na washirika wa sekta ya afya na maendeleo kuhusu hatua za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini, kwa lengo la kuimarisha mikakati ya kudhibiti maambukizi na kupata rasilimali zaidi.
Mkutano huo umeongozwa na Katibu Mkuu wa Afya ya Umma, Mary Muthoni, na kuwaleta pamoja wadau kutathmini hali ya ugonjwa huo, kubaini mahitaji ya dharura na kujadili changamoto za ufadhili.
Miongoni mwa washiriki ni washirika wa maendeleo katika sekta ya afya nchini Kenya DPHK, mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya afya HENNET, Shirikisho la Huduma za Afya Kenya KHF na Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya KRCS.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































