POLICE NA LEOPARDS KUKUTANA NYAYO
Kocha wa Kenya Police, Nicholas Muyoti, anakutana na klabu yake ya zamani AFC Leopards katika mechi ya Ligi Kuu ya FKF saa tisa alasiri katika uwanja wa Nyayo.
Police inalenga ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja na Migori Youth, huku Leopards ikitoka sare tasa dhidi ya Bandari.
Muyoti amesema bado ana imani na azma ya Police kutwaa taji la ligi, licha ya kupoteza pointi katika mechi ya ufunguzi, huku timu zote zikisaka ushindi ili kuimarisha kampeni zao za ubingwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































