RUTO AHIMIZA UBUNIFU NA TEKNOLOJIA KUKUZA UCHUMI
Rais William Ruto amewahimiza Wakenya kukumbatia ubunifu, teknolojia na vipaji ili kukuza uchumi na kujipatia uhuru wa kifedha, katika ujumbe wake wa Siku ya Mashujaa 2026.
Katika ujumbe wake Ruto amewapongeza wanaotumia vipaji na ubunifu kujitafutia riziki, akilinganisha juhudi zao na mapambano ya mashujaa wa taifa kupata uhuru.
Rais amesema uchumi wa ubunifu unaweza kufungua nafasi za ajira, kuongeza mapato na kuibua fursa mpya kwa vijana kupitia teknolojia na kazi za kidijitali.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































