#Local News

PKOSING AIBUA UTATA KWA KAULI KUHUSU UCHAGUZI WA 2027

Mbunge wa Pokot Kusini, David Pkosing, ameitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, kuondoa majina ya wagombea wengine wa urais katika uchaguzi wa 2027 na kubakiza jina la Rais William Ruto pekee, kauli iliyozua utata kuhusu ushindani wa kisiasa.

Matamshi hayo yanajiri huku washirika wa Ruto katika eneo la Bonde la Ufa wakizidisha juhudi za kuunga mkono azma yake ya kuchaguliwa tena, baadhi yao wakisisitiza kuwa ushindi wa 2027 lazima upatikane kwa vyovyote vile.

Kauli ya Pkosing imefuatia matamshi mengine yenye utata kutoka kwa Mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi na Seneta wa Nandi Samson Cherargei, waliotoa kauli za kumuunga mkono Ruto wakati wa ziara yake katika eneo la Bonde la Ufa Kaskazini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *