DEBORAH BARASA AMESEMA WAZEE WA VIJIJI WATAHUSISHWA KWA JUHUDI ZA SERIKALI ZA KUJIANDAA KWA MVUA ZA ELNINO
Waziri wa Mazingira Deborah Barasa amesema wazee wa vijiji wanahusishwa katika juhudi za serikali za kujiandaa kwa El Niño na kurejesha mazingira.
Barasa amesema wazee hao, ambao wana ushawishi mkubwa katika ngazi ya vijiji watasaidia kubaini maeneo yaliyo katika hatari ya mafuriko na maporomoko ya ardhi, pamoja na kuwashauri wananchi kuhusu hatua za kuchukua.
Amesema Kenya ina zaidi ya wazee wa vijiji elfu 77,000, huku wizara ikiwa imeandaa vijitabu vya kuwapa taarifa kuhusu urejeshaji wa mazingira, usafi, kuzuia uchafuzi na maandalizi ya majanga.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































