#Local News

MAHAKAMA KUU IMEMWACHILIA HURU INSPEKTA JENERALI WA POLISI DOUGLAS KANJA

Mahakama Kuu imemwachilia huru Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja katika kesi ya kukaidi amri ya mahakama kuhusu uwekaji wa vizuizi vya barabarani wakati wa maandamano ya Juni 25.

Kanja amefikishwa mahakamani Jumatatu kwa ajili ya kusikilizwa kwa hoja za hukumu baada ya Jaji Patricia Nyaundi kumpata na hatia ya kushindwa kuhakikisha maafisa walio chini yake wanatii amri hiyo.

Kanja ameandamana na maafisa waandamizi wa polisi akiwemo Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohamed Amin.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *