EQUITY HAWKS YACHAPWA NA APR 91-56
Matumaini ya Kenya katika mashindano ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa ya Mpira wa Kikapu Afrika kwa Wanawake, , yamepata pigo baada ya Equity Bank kufungwa 91-56 na APR ya Rwanda mjini Kibaha, Tanzania, Jumapili jioni.
APR ilianza kwa kasi na kushinda robo ya kwanza kwa pointi 18-9, huku Equity ikishindwa kuendana na kasi ya wapinzani wake.
Licha ya juhudi za Equity katika robo ya pili, APR iliendeleza ubabe na kuongoza kwa pointi 40-26 kuelekea robo ya tatu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































