DUALE ATAKA USHIRIKIANO ZAIDI KATIKA KUPATIKANA KWA DAWA BORA
Waziri wa Afya Aden Duale ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya serikali, wasambazaji na watoa huduma za afya ili kuhakikisha wagonjwa wanapata dawa bora kwa wakati.
Duale amesema Kenya bado inakabiliwa na changamoto ya kuwahakikishia wagonjwa upatikanaji wa dawa salama, zenye ufanisi na zinazoweza kumudu gharama, huku utekelezaji wa ajenda ya afya kwa wote ukiendelea.
Amesema ushirikiano kati ya wadau hao ni muhimu katika kuboresha upatikanaji wa dawa na kuhakikisha huduma za afya zinakidhi mahitaji ya wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































