KIMANI AFICHUA SIRI YA USHINDI WA EMERGING STARS DHIDI YA TANZANIA
Kocha mkuu wa Emerging Stars Anthony Kimani amesema kufahamiana kwa wachezaji pamoja na mchango wa kocha mwenye uzoefu Salim Babu vilichangia Kenya kuanza vyema kampeni ya kufuzu Kombe la Afrika la Mataifa kwa vijana chini ya miaka 23 mwaka 2027.
Kenya iliichapa Tanzania 4-1 katika Uwanja wa Nyayo Jumatatu, huku Kimani akisema maandalizi mazuri yaliwasaidia wachezaji kuzoeana haraka licha ya kuwa na muda mfupi wa pamoja.
Kimani amesema mwendelezo wa kikosi ulikuwa muhimu kabla ya mechi ya marudiano, huku benchi la kiufundi likiwachagua zaidi wachezaji waliowahi kucheza pamoja katika timu ya vijana chini ya miaka 20.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































