#Football #Sports

STARLETS YAFUNGA SEYCHELLES JUMLA YA MABAO 22-0

Timu ya taifa ya wanawake ya Kenya, Harambee Starlets, imeweka rekodi ya ushindi mkubwa zaidi kwa jumla baada ya kuichabanga Seychelles mabao 22-0 katika mechi mbili za kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles 2028.

Starlets ilirudia ushindi wa mabao 11-0 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Jumatatu katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex, na hivyo kufuzu kwa hatua inayofuata kwa kishindo.

Kenya sasa itakutana na Malawi au Zimbabwe katika raundi ijayo, huku Malawi ikiwa na faida ya mabao 2-0 kabla ya mechi ya marudiano mjini Harare Jumanne, baada ya dada wawili Temwa na Tabitha Chawinga kufunga mabao hayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *