KENYA YATHIBITISHA KESI YA PILI YA EBOLA
Kenya imethibitisha kisa cha pili cha Ebola, siku kumi baada ya mgonjwa wa kwanza kufariki dunia baada ya kusafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye ni jamaa wa karibu wa mgonjwa wa kwanza, alianza kuonyesha dalili akiwa karantini, hatua iliyowezesha wahudumu wa afya kumtambua mapema.
Maafisa wa afya wanasema ufuatiliaji wa watu waliokutana na wagonjwa pamoja na uchunguzi wa karibu umechangia kugunduliwa kwa kisa hicho, huku juhudi za kudhibiti maambukizi zikiendelea.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































