KNH YASAINI MAKUBALIANO MAPYA NA WAHUDUMU WA UUGUZI
Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Chama cha Kitaifa cha Wauguzi na Wakunga vimesaini makubaliano mapya ya kazi yatakayodhibiti ajira, mishahara na maendeleo ya kitaaluma kwa wafanyakazi wa kudumu na wa mikataba.
Makubaliano hayo yaliyotiwa saini hapo jana yanahusu kipindi cha mwaka 2025 hadi 2029, na yanawapa wauguzi marupurupu ya sare na huduma za uuguzi.
Pia yanaweka utaratibu wa wauguzi walioajiriwa kwa mikataba kuhamishiwa ajira za kudumu zenye mafao ya pensheni kuanzia Julai mosi, 2026.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































