HARAMBEE STARS YAFUNGWA NA GUINEA NA KUBAKI BILA USHINDI
Harambee Stars imepoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Guinea jijini Conakry Alhamisi, na kubaki bila ushindi baada ya mechi mbili za Kundi D katika mchujo wa Kombe la Afrika 2027.
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Serhou Guirassy alifunga bao pekee baada ya kuitumia vyema mpira uliomponyoka beki wa Kenya, na kuipa Guinea pointi zake za kwanza katika kampeni hiyo.
Kwa Kenya, matokeo hayo yanaifanya Harambee Stars kubaki bila ushindi katika mechi mbili mfululizo, baada ya kutoka sare ya 1-1 na Eritrea katika Uwanja wa Nyayo siku chache zilizopita.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































