#Local News

ZUBEIDA KANANU IMEZITAKA TAASISI ZA UMMA KUBORESHA UPATIKANAJI WA TAARIFA KWA UMMA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Rais wa Chama cha Wahariri Nchini Zubeidah Kananu ametoa wito kwa taasisi za umma kuboresha upatikanaji wa taarifa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 akisema hatua hiyo itasaidia kukabiliana na taarifa potovu na kuimarisha uadilifu wa uchaguzi.

Kananu amesema taarifa za wakati sahihi na zinazoaminika ni muhimu kwa wananchi kufanya maamuzi kwa ufahamu, pamoja na kuiwajibisha serikali na taasisi za umma.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa kwa Wote ya mwaka 2026, Kananu amezitaka taasisi za serikali kutoa taarifa kwa uwazi na kuhakikisha zinapatikana kwa urahisi kwa wananchi.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

ZUBEIDA KANANU IMEZITAKA TAASISI ZA UMMA KUBORESHA UPATIKANAJI WA TAARIFA KWA UMMA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

KANUNI MPYA ZA DENI ZA IMF ZAANGAZIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *