KENYA YAADHIMISHA MASHUJAA 264 WA TAIFA
Kenya imewatambua mashujaa 264 wa taifa katika maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Mashujaa, huku viongozi wakitaja mchango wao katika maendeleo ya nchi.
Mchambuzi wa siasa Fwamba NC Fwamba amesema tathmini ya serikali ya Rais William Ruto inapaswa kuzingatia utekelezaji wa miradi, akitaja ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, kupanua huduma za afya kupitia SHA na kuajiri zaidi ya walimu laki moja.
Fwamba pia ametaja mipango ya kuwezesha wananchi kupata ardhi kwa gharama nafuu, akisema hatua hizo ni sehemu ya rekodi ya utendakazi wa serikali badala ya ahadi pekee.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































