JUNIOR STARLETS YAELEKEA UHISPANIA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA
Timu ya Kenya ya wasichana walio chini ya miaka 17 Junior Starlets itaelekea Hispania kwa kambi maalum ya mazoezi kuelekea Kombe la Dunia la wanawake chini ya miaka 17 nchini Morocco.
Kenya itacheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Australia pamoja na vilabu vya uhispania Real Betis na Cádiz, hatua itakayosaidia benchi la kiufundi kuipima timu dhidi ya wapinzani wenye ushindani.
Baada ya kambi hiyo, Junior Starlets itasafiri moja kwa moja hadi Morocco ambako iko Kundi E pamoja na China, Marekani na Samoa, huku ikianza kampeni dhidi ya China Jumatatu Oktoba 19.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































