#Local News

SABINA CHEGE ALAANI UNAFIKI WA WANASIASA

Mbunge Mteule, Sabina Chege, amekosoa siasa za Kenya akisema wanasiasa hubadilisha misimamo na miungano kulingana na maslahi yao.

Chege amesema seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anapokaribishwa katika kundi la Wamunyoro huonekana kukubalika, lakini Ndindi Nyoro anapohusishwa na kundi hilo huitwa msaliti.

Ametaja hali hiyo kuwa unafiki wa hali ya juu, akisema wanasiasa wengi wanafanana licha ya kuwa katika makundi tofauti ya kisiasa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *