#Local News

PASSARIS AUNGA MKONO KIWANDA CHA MAFUTA DANGOTE

Mwakilishi wa  Wanawake kaunti ya Nairobi Esther Passaris ameunga mkono uwekezaji wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote nchini, akisema mradi huo unaweza kuleta manufaa kwa Kenya.

Passaris amesema serikali ya kitaifa na kaunti itahakikisha watu watakaopoteza ardhi yao kwa ajili ya mradi huo watalipwa fidia inayostahili, akisisitiza kuwa hakuna anayepaswa kupoteza mali yake bila fidia ya kutosha.

Amesema uwekezaji huo unapaswa kuendelea huku serikali ikichukua hatua zinazohitajika kuhakikisha walioathiriwa wanalindwa na kulipwa fidia ipasavyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *