#Local News

RUTO AMJIBU UHURU KUHUSU UCHAGUZI WA 2022

Rais William Ruto amepuuza matamshi ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kwamba uchaguzi wa mwaka 2022 uliibwa kwa manufaa yake.

Akizungumza katika Kaunti ya Taita Taveta, Ruto amemkosoa Uhuru kwa kurejelea suala hilo, akidai kuwa matamshi hayo ni ya uchochezi na ya kizembe.

Ruto amesisitiza umuhimu wa viongozi kuwa waangalifu wanapozungumzia masuala ya uchaguzi, akisema kauli zao zinaweza kuchochea hisia miongoni mwa Wakenya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *