GACHAGUA ASEMA MMOJA WA VIONGOZI WA UPINZANI ATAONDOKA.
Kiongozi wa Chama cha DCP Rigathi Gachagua amedai kuwa mmoja wa vinara wa muungano wa upinzani huenda akajiondoa iwapo hatateuliwa kuwa mgombea wa urais wa muungano huo katika uchaguzi wa mwaka 2027.
Akizungumza mjini Dallas, Texas, Gachagua amesema anaamini hata iwapo mmoja wa vinara hao ataondoka, upinzani bado unaweza kupata asilimia 75 ya kura na kumshinda Rais William Ruto.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































