#Local News

MBADI AUTETEA MRADI WA KIWANDA CHA MAFUTA LAMU

Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi ametetea mradi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote Lamu, akisema utakuwa na manufaa kwa Kenya licha ya upinzani unaoendelea kuhusu utekelezaji wake.

Mbadi amewatuhumu wanaodai fidia kuwa sehemu ya magenge ya uporaji wa ardhi yanayolenga kuipotosha serikali kupitia madai ya umiliki wa ardhi yasiyo ya kweli.

Waziri huyo pia amemtetea Rais William Ruto dhidi ya madai kuwa ana hisa katika mradi huo wa thamani ya shilingi trilioni mbili, akisema madai hayo hayana msingi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *