#Local News

KENYA YATHIBITISHA KISA KIPYA CHA EBOLA, IDADI YAFIKA NANE

Kenya imerekodi kisa kingine cha Ebola na kufikisha jumla ya visa vinane, huku Wizara ya Afya ikiimarisha hatua za kuwalinda wahudumu wa afya na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Afya, Dkt Patrick Amoth, amesema serikali imejiandaa vya kutosha kudhibiti maambukizi hayo, ambayo yamewaathiri zaidi wahudumu wa afya na jamaa wa karibu wa mgonjwa wa kwanza aliyefariki mapema mwezi huu.

Kisa hicho kipya kimetangazwa baada ya wizara kuthibitisha visa vinne vipya siku ya Jumamosi, na kufikisha idadi ya walioambukizwa saba kabla ya ongezeko hilo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *