RAGA: ADHIAMBO KUREJEA KWA LIONESSES
Mchezaji wa Kenya anayechezea Racing 92 nchini Ufaransa, Grace Adhiambo, anatarajiwa kurejea katika kikosi cha Kenya Lionesses kwa mashindano ya raga ya Afrika ya wachezaji saba kila upande, Novemba 7 na 8 katika uwanja wa RFUEA.
Adhiambo alikosa mashindano ya Safari Sevens kutokana na majukumu ya klabu, lakini anatarajiwa kujiunga na timu ya taifa wiki moja kabla ya mashindano hayo, huku Kenya ikilenga kuipiku Afrika Kusini na kupata nafasi ya kupanda daraja.
Kenya ilipoteza 22-0 dhidi ya Afrika Kusini katika fainali ya mwaka jana, na kocha Simon Odongo anaamini uzoefu na uwezo wa Adhiambo kupanga mashambulizi utasaidia timu kutwaa taji la Afrika na kufuzu kwa HSBC Sevens II.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































