#Local News

GAVANA ABDI GUYO AMESEMA YUKO TAYARI KUGHURA CHAMA CHA UDA NA KUWA MGOMBEA HURU WA UGAVANA

Gavana wa Isiolo, Abdi Ibrahim Guyo, amesema yuko tayari kuachana na tiketi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA) na kuwania kiti hicho kama mgombea huru, iwapo hatua hiyo itawazuia wapinzani wake wa kisiasa kuondoka katika kambi ya Rais William Ruto.

Guyo amesema ana imani atapata tiketi ya UDA ili kutetea kiti chake katika uchaguzi ujao. Hata hivyo, amewataka washindani wake kutotumia ushindani wa uteuzi wa chama hicho kama sababu ya kuachana na azma ya kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto na kujiunga na upinzani.

Akizungumza na wananchi wa Isiolo, gavana huyo amesisitiza kuwa mchakato wa uteuzi wa UDA utakuwa huru na wa haki. Aidha, amewataka viongozi kuweka mbele maslahi ya kisiasa ya Rais Ruto badala ya kutanguliza matarajio yao binafsi.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *