ONYONKA ATAKA MABADILIKO YA KATIBA KUKABILIANA NA UFISADI
Seneta wa Kisii, Richard Onyonka, ametaka marekebisho ya katiba ili kukabiliana na ufisadi, ukosefu wa usawa na kudhoofika kwa taasisi za serikali.
Onyonka amesema utamaduni wa siasa za mshindi kuchukua yote unakwamisha maendeleo ya usawa na kuchochea upendeleo wa kisiasa.
Amesisitiza kuwa rasilimali za umma na miradi ya serikali vinapaswa kugawanywa kwa haki badala ya kutumika kuwazawadia washirika wa kisiasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































