#Local News

JENGO LA GHOROFA NYINGI LILILOKUWA LIKIJENGWA LIMEPOROMOKA EASTLEIGH NAIROBI

Jengo la ghorofa nyingi lililokuwa likijengwa limeporomoka katika barabara ya 9, eneo la Eastleigh jijini Nairobi, huku kukiwa na hofu kuwa watu kadhaa huenda wamenasa chini ya vifusi.

Idadi ya watu walioathiriwa na tukio hilo bado haijabainika, huku shughuli za uokoaji zikitarajiwa kubaini iwapo kuna watu walionasa kwenye vifusi vya jengo hilo.

Walioshuhudia wamesema hali ya taharuki ilitanda eneo la tukio, huku baadhi ya watu wakianza kupora mali na kuwarushia mawe wahudumu wa magari ya kubeba wagonjwa. Hali hiyo ililazimu magari hayo kubadili njia kwa muda kabla ya kufika eneo la tukio kuanza shughuli za uokoaji.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *