KANJA AONYA POLISI WANAOWANYANYASA UMMA
Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amewaonya maafisa wanaohusika na utovu wa nidhamu kuwa watawajibika kwa matendo yao, kufuatia kushambuliwa kwa mwandishi wa habari jijini Nairobi alipokuwa akiripoti maandamano dhidi ya gharama ya juu ya mafuta.
Kanja amesema tukio hilo lililonaswa na kamera na kurushwa na vyombo vya habari limeichafua taswira ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi licha ya onyo za mara kwa mara kuhusu kudumisha weledi.
Onyo hilo linafuatia kushambuliwa kwa mwanahabari wa Royal Media Ode Francis na maafisa wa polisi siku ya Mashujaa alipokuwa akiripoti maandamano jijini Nairobi.
Imetayarishwa Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































