KAZI ZA MWISHO ZA TALANTA STADIUM ZAKAGULIWA
Kazi za mwisho na marekebisho katika uwanja wa Talanta Stadium zimekaguliwa huku Kenya ikiimarisha maandalizi ya kuandaa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027.
Katibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzi Patrick Mariru aliongoza kikao cha tathmini uwanjani Alhamisi akishirikiana na mwenzake wa Michezo Elijah Mwangi pamoja na maafisa wa Sports Kenya na Jeshi la Ulinzi la Kenya.
Mariru amesema kikao hicho kilijikita katika kazi zilizosalia na marekebisho yanayohitajika ili kuhakikisha uwanja huo unakidhi viwango vya Shirikisho la Soka Afrika kabla ya mashindano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































