ATWOLI APINGA AZMA YA SIFUNA KUWANIA URAIS
Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli, amepinga azma ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwania urais, akisema bado hajajiandaa kuongoza nchi
Akizungumza katika mazishi eneo la Kanduyi, kaunti ya Bungoma, Atwoli ametangaza kumuunga mkono Rais William Ruto kuchaguliwa tena mwaka 2027, huku akionya Jamii ya Waluhya dhidi ya kutumiwa kisiasa na viongozi vijana
Atwoli pia amekosoa uhusiano wa Sifuna na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































