MBADI ATUPILIA MBALI MADAI YA NYORO KUHUSU KPC
Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi amepuuzilia mbali madai ya kiongozi wa People’s Party of Kenya, Ndindi Nyoro, kuwa Rais William Ruto anapanga kutwaa kampuni ya Kenya Pipeline kupitia bilionea wa Nigeria Aliko Dangote.
Mbadi amesema uuzaji wa asilimia 25 ya hisa za kampuni hiyo ulikuwa shughuli halali ya kibiashara kati ya muuzaji aliyejitolea kuuza na mnunuzi aliyejitolea kununua.
Waziri huyo amemtaka Nyoro kukoma kutoa matamshi ya kisiasa yanayoweza kuwatia hofu wawekezaji wa kigeni na kuhatarisha imani yao katika soko la Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































