EPL: CHELSEA vs TOTTENHAM
Ligi Kuu ya Uingereza inaendelea leo usiku kwa mechi kati ya Ipswich Town na Nottingham Forest itakayochezwa saa nne usiku.
Kesho, Aston Villa itamenyana na Manchester City saa nane unusu, huku Coventry ikikabiliana na Fulham na Arsenal ikiikaribisha Everton saa kumi na moja jioni, kabla ya Chelsea kukutana na Tottenham saa moja unusu usiku.
Jumapili, Liverpool itamenyana na Brighton, Manchester United ikikabiliana na Bournemouth, huku Crystal Palace ikiikaribisha Newcastle mechi zote zikianza saa kumi na moja jioni.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































