#Local News

RAIS RUTO ASAINI SHERIA MPYA YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

Rais William Ruto amesaini Mswada wa watu wenye mahitaji maalum wa mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika Ikulu, Nairobi.

Amesema sheria hiyo ni hatua ya maendeleo inayothibitisha haki na utu wa watu hao, sambamba na Ibara ya 54 ya Katiba ya Kenya.

Sheria mpya inapiga marufuku ubaguzi na kutaka mazingira ya umma, usafiri na teknolojia ya mawasiliano yafikiwe kwa urahisi na watu wote.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *