SERIKALI YASHUTUMIWA KUHUSU “UDHALIMU WA TANZANIA”
Serikali imeendelea kushutumiwa kwa jinsi ilivyoshughulikia suala la utekaji nyara na madai ya unyanyasaji dhidi ya mwanaharakati Boniface Mwangi nchini Tanzania, na jinsi ilivyounga mkono kufurushwa kwa mawakili na wanaharakati kutoka nchini humo.
Kwenye mahojiano na runinga moja nchini, viongozi mbali akiwemo mbunge wa Kitui Central Makali Mulu, mwenzake wa Uriri Mark Nyamita na mtaalam wa masuala ya kisiasa Billow Kerrow, wameitaka jamii ya kimataifa kuiwajibisha serikali ya Tanzania.
Kauli yao imejiri chini ya siku moja baada ya Mwangi na mwanahabari Agather Atuhaire wa Uganda kudai kwamba walifanyiwa madhila kadhaa ikiwemo kudhulumiwa kingono nchini humo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































