BUNGE KUCHUNGUZA USAMBAZAJI WA CHANJO
Kamati ya afya bungeni chini ya uongozi wake mbunge wa seme James Nyikal imeanzisha uchunguzi katika usambazaji wa chanjo aina ya BCG na ile ya polio katika maeneo tofauti na itawasilisha ripoti yake bungeni katika muda wa juma moja.
Ni agizo lililotolewa na spika wa bunge la taifa Moses Wetangula kufuatia uhaba wa chanjo hizo akisema huenda hali hiyo ikaathiri watoto wanaozaliwa na jamii zilizotengwa.
Hata hiyo wizara ya afya inasema chanjo zaidi zimewasili na zitaanza kusambazwa hivi karibuni.
Imetayarishwa na Maureen Amwai
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































