OBILO KUTUMIA MECHO ZILIZOSALIA KUJIANDAA KWA MSIMU UJAO
Kocha Mkuu wa Zetech Sparks Maurice Obilo atatumia mechi zilizosalia za msimu wa kawaida kama maandalizi ya mchujo ujao, katika Ligi Kuu ya kitaifa ya Kikapu ya Wanawake nchini.
Wanafunzi hao walilaza Stanbic Aces 53-37 kabla ya kupata ushindi mwingine wa 63-56 kwa wenzao wa vyuo vikuu Strathmore Swords wikendi katika uwanja wa Nyayo na Ulinzi Sports Complex mtawalia.
Licha ya kushinda mara mbili wikendi iliyopita, Maurice Obilo anakiri kuwa haikuwa rahisi.
Zetech Sparks hadi sasa wanaongoza ligi ya wanawake wakiwa na pointi 38 wakiwa wamecheza michezo 20, wakishinda 18 na kupoteza miwili.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































