MAGAVANA KUJADILI EGP JUMATATU
Magavana wameratibu mkutano maalum hii leo kujadili mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki ambao umezinduliwa na serikali kuu, wakisisitiza kuwa changamoto zilizo kwenye mfumo huo ni sharti ziangaziwe kabla yao kuukumbatia.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la magavana Ahmed Abdullahi, magavana wamepinga dhana kwamba wanapinga mfumo huo, licha ya serikali kuu kushikilia kwamba ni sharti mfumo huo utekelezwe.
Kulingana na serikali kuu, mfumo huo unalenga kudhibiti ufisadi katika ununuzi na utoaji wa kandarasi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































