EQUITY YAAHIDI MAPAMBANO MAKALI DHIDI YA GSU NYAYO
Kocha mkuu wa timu ya mpira wa mkono ya Equity, Peter Mwathi,
amesema hawatamdharau kabisa General Service Unit (GSU)
watakapokutana Jumamosi katika mechi inayosuburiwa kwa hamu
kwenye uwanja wa Nyayo.
Equity wataingia uwanjani wakilenga kuendeleza ubabe wao dhidi ya
kikosi hicho cha para-military, lakini Mwathi anasisitiza kuwa
tahadhari ni muhimu licha ya kujiamini kuelekea mtanange huo.
Kikosi hicho kilichomaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita hakitaki
kupoteza nafasi yoyote msimu huu, kikilenga kuwania taji tena, na
GSU ndiyo itakuwa jaribio la kwanza muhimu kwa Mwathi katika
kampeni za msimu huu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































