NTSA YAWAONYA MADEREVA KUHUSU ULAGHAI
Mamlaka ya usalama barabarani NTSA imewatahadharisha madereva kuhusiana na kundi la wahalifu linalojifanya maafisa wa NTSA na kuitisha faini kupitia SMS kutoka kwa madereva kwa misingi kwamba madereva hao wamevunja sheria za trafiki.
Kupitia notisi, NTSA imesema washukiwa wamekuwa wakituma tovuti kupitia SMS kuwaelekeza madereva namna ya kulipa faini zinazodaiwa.
Mamlaka hiyo imejitenga na tovuti hiyo, na kuwaonya madereva dhidi ya kulipa faini kupitia tovuti hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































