#Local News

MAAFISA WA KLINIKI WAANZA MGOMO

Huduma za matibabu kote nchini zinakabaliwa na hatari ya kusambaratika kutokana na mgomo wa maafisa wa kliniki ambao umeanza usiku wa kuamkia leo kuhusiana na mzozo wa malipo ya maafisa hao.

Chini ya muungano wao KUCO, maafisa hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Peterson Wacira na katibu mkuu George Gibore, wameendelea kumkosoa Waziri wa afya Aden Duale kwa kukosa kutia saini mkataba wao wa maelewano ambao ungefanikisha ulipaji wa malipo yao.

Wizara ya afya na serikali za kaunti zilisusia mkutano wa hapo jana.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAAFISA WA KLINIKI WAANZA MGOMO

WAKENYA WALIOKWAMA MYANMAR WAREJESHWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *