JESHI LA VENEZUELA LAMTAMBUA KIONGOZI MPYA
Jeshi la Venezuela limetangaza kumuunga mkono aliyekuwa makamu wa Rais Nicolas Maduro aliyebanduliwa na Marekani, Delcy Rodriguez kuwa rais wa taifa hilo baada ya kuapishwa.
Waziri wa ulinzi nchini humo Vladimir Padrino Lopez ameashiria kumuunga mkono Rodriguez ambaye rais wa Marekani Donald Trump amesema ni kiongozi mwafaka ambaye Marekani inaweza kufanya naye kazi.
Kupitia hotuba katika runinga ya kitaifa, Padrino amewahimiza wananchi kurejelea maisha yao ya kawaida huku kukiwa na suitofahamu kuhusu mustakabali uongozi wa taifa hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































