KESI YA SALASYA- NCIC YAAHIRISHWA
Mahakama kuu jijini Nairobi imeahirisha kupitishwa kwa makubaliano ya suluhu katika kesi inayomhusisha mbunge wa Mumias East Peter Salasya na tume ya kitaifa ya uwiano na utangamano NCIC ambako Salasya anatuhumiwa kutoa matamshi ya chuki.
Hii ni baada ya mahakama kufahamishwa kwamba baadhi ya vigezo vya makubaliano hayo havijaafikiwa, ambako mbunge huyo anafaa kupewa wajibu kadhaa wa kuhakikisha uwiano na amani.
Mahakama hiyo imempa mbunge huyo muda wa kutii vigezo hivyo kabla ya uamuzi wa kuondoa mahakamani kesi yake kutolewa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































