VIONGOZI WAONYWA DHIDI YA SIASA KWENYE OPERESHENI LA USALAMA
Serikali imewaonya viongozi dhidi ya kuingiza siasa kwenye operesheni ya kuwakabili wezi wa mifugo katika eneo la Kaskazini mwa bonde la ufa kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza katika eneo la Kapsowar kaunti ya Elgeyo Marakwet, Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, amewahakikishia wakazi kwamba utulivu utarejea hasa mpakani mwa kaunti za West Pokot na Elgeyo Marakwet.
Aidha, ameahidi operesheni kwenye msitu wa Mkokodo kaunti ya Meru.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































