#Football #Sports

BINGWA KABRAS ATINGA NUSU FAINALI ENTERPRISE CUP

Mabingwa watetezi Kabras RFC wamefuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Enterprise baada ya kupewa ushindi wa mezani dhidi ya Kenya Harlequins, ushindi uliorekodiwa rasmi kama pointi 48–13. Mchezo huo ulikuwa umepangwa kuchezwa Jumamosi katika uwanja wa ASK Showgrounds mjini Kakamega., ila Harlequins wakakosa kufika uwanjani.

Msimu huu wa Kombe la Enterprise umejaa changamoto nyingi, huku timu kadhaa zikishindwa kutimiza ratiba ya mechi zao, hali ambayo imesababisha kuwepo kwa ushindi wa mezani mara kwa mara, na hivyo kuwapa wapinzani wao tiketi ya kusonga mbele pamoja na pointi bila kupambana uwanjani.

Kabras RFC, Menengai Oilers na Nakuru RFC zote zilifuzu robo fainali kupitia ushindi wa mezani dhidi ya Impala Saracens, Masinde Muliro University na South Coast Pirates mtawalia.

Kocha mkuu wa Kabras RFC Carlos Katywa alikosoa vikali mpangilio wa mashindano hayo, akisema klabu hazikushirikishwa vya kutosha kabla ya ratiba ya mechi kutolewa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

BINGWA KABRAS ATINGA NUSU FAINALI ENTERPRISE CUP

“NAIROBI UNITED JOGOO LA SHAMBA”

BINGWA KABRAS ATINGA NUSU FAINALI ENTERPRISE CUP

DAYSTAR FALCONS WAJIOKOA NA MMUST

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *