BENNI MCCARTHY AONYESHA DALILI ZA KUONDOKA STARS
Kocha wa timu ya taifa ya Harambee Stars, Benni McCarthy, amesema anahisi hajatumika ipasavyo katika nafasi yake, akitaja mpangilio usiokamilika wa mechi za kimataifa kama chanzo cha kutoridhika kikazi.
McCarthy, raia wa Afrika Kusini na mshindi wa UEFA Champions League na FC Porto, amesema kuwa anafurahia kuhusiana na wachezaji kila siku, jambo ambalo usimamizi wa timu ya taifa mara nyingi hauwezeshi.
Kocha huyo aliteuliwa kuongoza Harambee Stars Machi 2025, tukio lililoleta matarajio makubwa katika soka la Kenya, huku mchezaji mwenye uzoefu wa juu barani Ulaya akiingia katika timu ya taifa yenye malengo ya mabadiliko makubwa
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































